Jeshi la Yanga ‘full’ muziki leo

NA WINFRIDA MTOI WACHEZAJI wa Yanga waliokuwa wanashiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, leo wanatarajia kuungana na wenzao katika mazoezi yanayoendelea katika Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini, Dar es Salaam. Kikosi cha Yanga kilitolewa katika hatua ya makundi ya mashindano hayo, baada ya kufungwa mechi mbili na kushinda mbili kati ya nne walizocheza. Akizungumza na BINGWA jana, Mratibu wa timu ya Yanga, Hafidh Saleh, alisema wachezaji hao waliwasili juzi na kupewa mapumziko ya siku moja, hivyo leo wataungana na wengine kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Tanzania...

read more...

Share |

Published By: Bingwa - 4 days ago

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News