Mkongwe awapa Man United beki

MANCHESTER, England KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Darren Fletcher, ameiambia timu hiyo ifanye haraka kumsajili beki wa kati wa Stoke City, Nathan Collins, mwenye umri wa miaka 18. Beki huyo alichaguliwa katika kikosi bora cha msimu katika Ligi Daraja la Kwanza, hiyo inaweza kumfanya kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, kushawishika kumsajili. Fletcher amekuwa shabiki mkubwa wa beki huyo ambaye anatajwa kuwaniwa na timu mbalimbali za Ligi Kuu zikiwamo Arsenal, Manchester City na Chelsea. Solskjaer anataka kuijenga Manchester United kwa kusajili wachezaji chipukizi ambao wataishi kwa muda mrefu...

read more...

Share |

Published By: Bingwa - Tuesday, 21 May

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News