Ajib arudi Yanga 

NA ZAITUNI KIBWANA NAHODHA wa Yanga, Ibrahim Ajib na beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’, wamerejesha tabasamu la mashabiki wa timu hiyo, baada ya kuungana na nyota wengine kwenye safari ya mkoani Morogoro. Yanga leo itasafiri na wachezaji 20 kuelekea Morogoro kuvaana na Mtibwa Sugar, katika mchezo wa Ligi Kuu utakaochezwa keshokutwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Ajib alikosekana katika kikosi hicho kwenye michezo mitatu ya timu hiyo, akiuguza jeraha la nyonga, huku Ninja akikosekana kwa kutumikia adhabu ya kufungiwa michezo mitatu. Akizungumza na BINGWA jana, Mratibu wa timu hiyo, Hafidhi Saleh, alisema...

read more...

Share |

Published By: Bingwa - Monday, 15 April

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News