Aliyedaiwa kuiba Sh mil saba kila dakika afutiwa kesi, akamatwa tena

Kulwa Mzee, Dar es Salaam MFANYABIASHARA aliyedaiwa kuiibia Serikali Sh milioni saba kwa kila dakika moja, Mohamed Yusufali na wenzake wanne walifutiwa kesi hiyo iliyowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kisha wakakamatwa tena jana na kusomewa upya mashtaka 39 likiwamo la kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni mbili. Washtakiwa hao walifutiwa kesi hiyo  baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuomba kuondoa shtaka hilo mahakamani hapo na hawana nia ya kuendelea nalo. Maombi hayo yaliwasilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Hashimu Ngole, kisha mahakama hiyo ikayakubali na washtakiwa wakafutiwa mashtaka...

read more...

Share |

Published By: Mtanzania - 7 days ago

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News