Amunike ndiyo basi tena Taifa Stars

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’  Emmanuel Amunike. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF leo Julai 8, imesema makubaliano hayo yamekuja baada ya pande zote mbili kufikia muafaka wa kusitisha mkataba wa kocha huyo raia wa Nigeria. TFF itatangaza kocha wa muda atayekiongoza kikosi cha Taifa Stars katika mechi za CHAN. “Makocha wa muda watatangazwa baada ya kamati ya dharura ya kamati ya utendaji itakapokutana Julai 11, mwaka huu,”...

read more...

Share |

Published By: Mtanzania - Monday, 8 July

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News