Bashungwa, Kichere kuapishwa kesho

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Rais Dk. John Magufuli anatarajia kuwaapisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Charles Kichere kesho Jumatatu Juni 10, Ikulu jijini Dar es Salaam. Hatua hiyo inatokana na mabadiliko madogo ya mawaziri ambapo alitengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda na kumteua Bashungwa ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo. Pia Rais Magufulu alitengua uteuzi wa Kichere aliyekuwa Kamishna Mamlaka ya Mapato (TRA), ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Njombe. Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi...

read more...

Share |

Published By: Mtanzania - 7 days ago

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News