Chadema wataka polisi imwachie Naibu Katibu Mkuu wao

Asha Bani, Dar es Salaam Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimelitaka Jeshi la Polisi kutoa taarifa rasmi juu ya tukio la kukamatwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu na wanachama wengine na kuwaachia huru mara moja. Jeshi la Polisi mjini Mafinga, mkoani Iringa, linamshikilia Mwalimu baada ya kumkamata mchana wa leo Jumapili Desemba 16, alipokuwa akiwasili kuongoza kikao cha ndani cha chama mjini hapo. Taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene, zimeeleza kusikitishwa kwao huku wakilitaka jeshi hilo kuwaachia huru...

read more...

Share |

Published By: Mtanzania - Sunday, 16 December

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News