DC ashinda kura za maoni jimbo la Lissu

Nathaniel Limu-SINGIDA WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Singida Mashariki, wamepiga kura kupata mwana CCM mmoja ambaye atapeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Julai 31. Katika mkutano huo uliofanyika jana, wanachama 13 walichuana katika uchaguzi huo na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu, ameongoza kura za maoni kwa kupata kura 396. Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Tundu Lissu kupoteza sifa. Mbali ya Mtaturu, wana-CCM wengine waliochuana katika kura hizo za maoni ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa...

read more...

Share |

Published By: Mtanzania - Thursday, 11 July

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News