Diwani Mwingine CHADEMA Atimkia CCM

Diwani wa kata ya Kianyari wilayani Butiama, Mugingi Muhochi (Chadema) amejiuzulu wadhifa wake na kujiunga na CCM.Akizungumza leo Septemba 11 Muhochi amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuridhishwa na utekelezaji wa ilani ya CCM chini ya Mwenyekiti wa CCM, Taifa, John Magufuli.Muhochi ambaye katika Uchaguzi Mkuu uliopita aligombea udiwani kupitia CCM lakini alishindwa katika kura za maoni za chama hicho na kuamua kujiunga na Chadema. Baada ya kujiunga na Chadema, alishinda udiwani kata ya Kianyari.Muchochi amesema ameamua kurudi CCM kwa hiari yake mwenyewe na bila kushawishiwa na mtu yeyote.Amesema katika...

read more...

Share |

Published By: Mpekuzi Huru - Tuesday, 11 September

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News