Frank Lampard amtaka Drogba Chelsea

LONDON, ENGLAND KOCHA wa Derby, Frank Lampard  wakati wowote kuanzia sasa anayetarajia kusaini mkataba wa kuinoa Chelsea, inaelezwa amemtaja mshambuliaji wa zamani klabuni hapo, Didier Drogba kutaka kufanya naye kazi katika benchi lake la ufundi. Lampard anapewa nafasi  hiyo kubwa ya kuchukua mikoba ya Maurizo Sarri anayetimkia Juventus, baada ya kukiongoza kikosi hicho msimu mmoja pekee na kufanikiwa kukiwezesha kutwaa  ubingwa wa Ligi ya Europa.  Mchezaji huyo wa zamani klabuni hapo, amebakiza mkataba wa mwaka mmoja pekee na waajiri wake wa sasa Derby, ambao wanahitaji kiasi cha Pauni milioni nne...

read more...

Share |

Published By: Mtanzania - Sunday, 16 June

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News