Marekani Yakasirishwa na vitisho vya Iran

Marekani haijafurahishwa na vitisho vilivyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif katika mkutano na mwenzake wa Ujerumani Heiko Maas mjini Tehran. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Kigeni ya Marekani amesema kuwa Iran inachagua moja rahisi tu, ijionyeshe kuwa nchi ya kawaida au ishuhudie uchumi wake ukisambaratika. Zarif aliituhumu Marekani kwa kufanya vita vya kiuchumi kutokana na vikwazo ilivyoiwekea Iran na akaonya kuwa wale wanaounga mkono vita wasitarajie kuwa salama. Maas anataka kuyaokoa makubaliano ya nyuklia na Iran, lakini hakupiga hatua zozote za maana...

read more...

Share |

Published By: Mpekuzi Huru - 5 days ago

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News