Rais Magufuli Aagiza Waziri Ambaye Jengo Lake Halijakamilika Dodoma Ahamie Hivyo Hivyo

Rais John Magufuli ameiagiza Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) inayoongozwa na Seleman Jafo kuhamia katika jengo la ofisi yao ‘pagale’ ambayo haijakamilika hivyo hivyo.Rais Magufuli alitoa agizo hilo jana ikiwa ni muda mfupi baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kueleza kuwa alikuwa na makubaliano na mawaziri kuwa siku majengo hayo yakizinduliwa mawaziri wangehamia.Hata hivyo, Majaliwa alimweleza Rais kuwa kuna baadhi ya wizara ikiwemo Tamisemi ambazo majengo yao yamechelewa kukamilika kutokana na kuchelewa kupata fedha.Waziri Mkuu alitaja muda ambao majengo hayo yatakamilika...

read more...

Share |

Published By: Mpekuzi Huru - Sunday, 14 April

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News