Sababu za Mbunge wa Temeke kujiuzulu akiwa bungeni

Fredy Azzah, Dodoma Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea (CUF), ametangaza kujivua unachama wa chama chake na kujiuzulu ubunge, akitaja sababu kuwa ni mgogoro kati ya wanachama wanaomtambua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mwenyekiti wa chama hicho na wale wanaomtambua Maalimu Seif Shariffu Hamad, kuwa Katibu Mkuu. Tofauti na wabunge wengine, Mtolea alitangaza uamuzi wake ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wabunge wakijadili Muswada wa Sheria Ndogo ya Fedha wa mwaka 2018. “Sijui mnaoshangilia mnashangilia nini, lakini tulio ndani ndiyo tunaujua huu mgogoro, imefikia hadi hatua ya kutishiana maisha huko mitaani,” amesema...

read more...

Share |

Published By: Mtanzania - Thursday, 15 November

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News