Sudan: Kiongozi wa baraza la mpito ajiuzulu

Waziri wa Ulinzi aliyeapishwa Alhamisi kuwa rais wa baraza la mpito la kijeshi Ahmed Awadh Auf amejiuzulu wadhifa huo na nafasi yake kuchukuliwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan Abdulrahman. Awadh Auf ametangaza hatua hiyo siku moja baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani rais al-Bashir na yeye kushika hatamu. Kwenye hotuba yake ya kujiuzulu, iliyorushwa kwenye televisheni Awadh Auf alisema anaachia wadhifa huo kwa maslahi ya taifa na kwa kuwa taifa hilo lina watu wazuri na jeshi la kuaminika. Amesema ana imani kwamba makundi hayo mawili yatafanya kazi pamoja. Jeshi...

read more...

Share |

Published By: Mtanzania - Sunday, 14 April

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News