Ufaransa Yapinga Matokeo ya Urais DRC

Ufaransa imepinga matokeo ya uchaguzi wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikisema ushindi uliotangazwa kwa kiongozi wa upinzani, Felix Tshisekedi haulingani na matokeo ambayo mpinzani wake mkubwa, Martin Fayulu anaonekana kuupata.Katika tamko lililotolewa jana baada ya matokeo ya awali kutangazwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian alisema Fayulu, ambaye alitangazwa kushika nafasi ya pili, ndiye aliyetakiwa kutangazwa mshindi."Kwa kweli inaonekana matokeo yaliyotangazwa, hayaendani na matokeo halisi," alisema alipozungumza na kituo cha televisheni cha CNews."Kwa kuangalia (matokeo halisi), Fayulu ndiye kiongozi aliyepatikana katika uchaguzi huu....

read more...

Share |

Published By: Mpekuzi Huru - Thursday, 10 January

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News