Viongozi watatu wa kijeshi wajiuzulu Sudan

Viongozi watatu wa Baraza la Uongozi wa Kijeshi wamejiuzulu nchini Sudan kufuatia baraza hilo kusema limefikia makubaliano kuhusu madai mengi ya viongozi wa maandamano wanaotaka serikali ya kiraia. Baraza hilo lenye wajumbe 10 liliwaalika viongozi wa maandamano kwa mazungumzo baada ya waandamanaji hao kuahirisha mkutano wa Jumapili na viongozi wa kijeshi. Msemaji wa baraza hilo la kijeshi Luteni Jenerali Shamseddine Kabbashi hakutoa maelezo zaidi juu ya madai makubwa ya waandamanaji hao ya kutaka serikali ya kiraia lakini amesema hakuna tena mzozano mkubwa kati yao. Mmoja wa viongozi hao wa maandamano...

read more...

Share |

Published By: Mtanzania - Thursday, 25 April

Toa Maoni yako hapa - Add your comment

 

Related News